0

Ratiba ya Kongamano kubwa la Vijana na Wazazi | Summit

Tarehe 14-15 Desemba

Haijalishi umetengeneza pesa kiasi gani, kama watoto wako wataharibika, wavute bangi, watumie madawa ya kulevya, wajiingize kwenye vitendo vya kihuni, wakatae shule, wakate tamaa ya kuishi, wawe majambazi au waugue magonjwa hatari kama HIV AIDS huwezi kuwa na furaha. Msaidie mwanao ili maisha yake yasije yakakugharimu amani yako, furaha yako na pesa zako. Jisajili sasa wewe na mwanao/wanao kushiriki katika Kongamano muhimu kwako na familia yako (Kongamano la Vijana na Wazazi), litakalofanyika siku ya tarehe 14 na 15 Dec. 2018 pale APC Hotel and Conference Centre Dar es Salaam kuanzia saa 2:00 asubuhi mpaka 12:00 jioni.

 

Kutakuwa na madarasa ya pamoja (vijana na wazazi) darasa la vijana peke yao, darasa la wazazi peke yao, wakati wa kukutana na washauri “professional counselors” na wakati wa michezo mbalimbali. Ratiba kamili, mada na walimu imeambatanishwa katika ujumbe huu. Gharama za ushiriki ni Tsh. 100,000/= kwa siku zote mbili zikijumuisha masomo, chakula, ushauri wa kitaalam “professional counseling” na michezo mbalimbali. Kununua tiketi yako piga simu namba 0714 508508. Sambaza ujumbe hii katika “whatsapp groups” za familia, shule, watu unaowajali na kuwatakia mema na yoyote unayeamini anathamini maisha ya watoto wake na familia yake, na Mungu atakubariki kwa kuokoa maisha ya mtoto/kijana/mzazi au familia-Paul R.K Mashauri

 

Follow us on our social accounts:
Tags:

Leave a Reply