Mbelwa Kairuki welcomes Silkroad Group to invest in Tanzania

Mbelwa Kairuki Ambassador Embassy of the United Republic of Tanzania

“Jukwaa la Biashara kwa njia ya mtandao (DODR Silk Road Cross Border Duty Free & Digital Trade Centre) limezinduliwa leo jijini Nanjing katika Jimbo la Jiangsu. Jukwaa hilo limeanzishwa na Kampuni ya China Silkroad Group na litatumika kuuza bidhaa za nje katika soko la China Katika hotuba ya ufunguzi wa Jukwaa hilo, Mwenyekiti wa China Silkroad Group Ndugu YAN Lijin ameeleza kwamba jukwaa hilo lina uwezo wa kuunganishwa na Majukwaa ya biashara ya nchi za nje (E-commerce platforms) ili bidhaa za nje ziuzwe katika soko la China Katika hafla hiyo, Balozi Kairuki ameikaribisha Kampuni ya China Silkroad Group kuwekeza nchini Tanzania katika uongezaji wa thamani ya bidhaa za kilimo, samaki, nyama na madini ili ziweze kuuzwa katika soko la China kupitia Jukwaa la Silk Road Cross Border Digitial Trade Centre”

Back to M

Follow us on our social accounts:
Verified by ExactMetrics